in

CoolCool LoveLove CuteCute LOLLOL OMGOMG WTFWTF CryCry AngryAngry

Jinsi ya Kuandika Makala Kitaalam.

Habari, Karibu katika blog yetu ya Swahilify.

Hii ni makala yangu ya kwanza katika blogi hii, tulikua na mtiririko wa kitu gani tutakacho ona kinafaa kutangulizwa na kuwasilishwa katika blogi hii, na kwakweli kwa blogi yenye kategoria pana inakua vigumu kujua wapi kwa kuanzia.

Mimi naitwa Mr.Admin na ntakua muhusika mkuu wa kuhakikisha mambo yote kwenye blogi yetu ya Swahilify yanaenda vizuri.

Kama bado hujatambua dhumuni la blogi hii tafadhali tembelea kurasa hii unapate kujifunza zaidi (Tambua).

Wakati tulikua na mawazo ya kitu gani cha kukiwasilisha, tukaona ni vyema kuwaelekeza watumiaji wa mtandao hasa tovuti hii njia mbali mbali zinazoweza kukuza sanaa ya mtandao.

Katika uchambuzi wa nini cha kuanzia nilipata mawazo ya kuwaelezea ni jinsi gani unavoweza ukaandika makala nzuri ya kitaalam. Hivyo basi pamoja na uzoefu nilifanya uchunguzi ili kuweza kutambua makala ya kitaalam ikoje na unaweza ukaindika kwa njia gani.

Jinsi ya Kuandika MAKALA Kitaalam

Tambua ya kuwa miundo ya kuandika Makala ipo ya aina tofauti, ila zote zina mfumo au njia zinafwata. Waandika makala wakubwa hua wana njia ambayo hutumia kuandika makala zao.

Kulingana na umakini wako, mbinu yako, makala yako inaweza kuwa na tofauti kidogo, lakini katika hayo kuna mbinu ambayo yanaweza fanya machapisho au makala kuwa na nguvu sana na muonekano mzuri. Mbinu hizo chache unaweza fuata ni..

 

1. Kichwa cha habari kinachovutia.

Ikiwa unataka kuandika makala kubwa kwa ajili ya blogi, tumia wakati kuunda kichwa cha habari, kinachowavutia wasomaji, na kuwaacha wakitamani ushauri, au maelekezo yako. “Hii ni hatua ya kwanza (na ya mwisho) kabla ya kuchapisha makala.”

Vitu vya kuzingatia katika kuandika kichwa cha habari:

a. Chagua mada yenye mvuto

Hakikisha mada utakayoiwasilisha iwe na wasomaji na hao watajisikia kulazimishwa kubonyeza na kupata suluhisho la kile wanachokipenda au kuwasumbua.

b. Chambua makala za watu wengine

Kuchunguza makala za wengine zinakupa muongozo wa kile ambacho wewe una mpango wa kukiandika.

c. Onjesha

Kichwa cha habari kinapaswa kimpe msomaji hamasa ya kuja kusoma makala yako. Usimpe msomaji majibu kwenye kichwa cha habari.

d. Punguza maneno, weka maneno yenye mvuto zaidi.

Kichwa chako cha habari kifanye kuwa kifupi na chenye nguvu iwezekanavyo. Ondoa maneno dhaifu na weka maneno ya nguvu yenye msisimko.

 

2. Andika utangulizi wenye msisimko

Inapokuja kwenye mtandao – urefu wa umakini wa watu ni mdogo zaidi kuliko makala ya kuchapishwa, hivyo aya yako ya ufunguzi ni muhimu. Waandishi wa habari wanalitambua hili. Msomaji huanza kuridhishwa na maelezo ya mwanzo wa makala na maelezo hayo humfanya msomaji aendelee kusoma.

Vitu vya kuzingatia katika kuandika utangulizi

a. Ingia kwenye akili ya msomaji

Ingia ndani ya viatu vyao na uandike kutoka kwa au kulingana na mtazamo wao. Waonyeshe unaelewa vizuri wanayopitia. Tambua nia ya msomaji kama vile wewe ni msomaji.

b. Washawishi wasomaji waendelee kusoma

Kadri msomaji anavyoendelea kusoma makala yako, ndivyo anavyozidi kupata nia ya kuendelea kusoma makala zako

c. Mfanye msomaji ajue kuwa atapata majibu.

Wasomaji wana wasiwasi gani? Je! Wanajua nini kitatokea ikiwa hawatatatua shida ambayo makala linashughulikia? Je! hali mbaya au nzuri zaidi ni ipi?

d. Muoneshe msomaji nchi ya ahadi ilipo.

Muelekeze msomaji wako kuwa kuna mwelekeo wa kile anachohitaji kusoma au kuelezewa na kwamba ataweza kukipata akiendelea kusoma makala yako.

 

3. Wasilisha kile ulichokusudia kukielezea

Ulipata wasomaji kubonyeza kwenye kichwa chako cha habari, ukawavuta kwa utangulizi, na sasa ni wakati wa kutekeleza yote uliyoahidi.

Kila hadithi unayosimulia au wazo unaloshiriki inahitaji kuwa na hoja inayounga mkono, jambo ambalo wasomaji wanaweza kung’ata. Fikiria kile unachotaka kusema na jinsi utakavyounga mkono. Njia nzuri ya kuandaa ni kutengeneza orodha.

Wakati unawasilisha zingatia yafuatayo

a. Weka kichwa kidogo cha habari baada ya aya kadhaa

Kwanini? Kwasababu vinamuongoza na kumfanya msomaji aelewe kirahisi yale uliozungumzia au kuelezea.

Endapo wasomaji wataona maandishi mengi wanapokuwa wakisoma bila kusimama kwa kutosha, watahisi kuwa wamezidiwa. Ni kama kwenda kwenye safari ya basi na kuambiwa hakutakuwa na mapumziko ya bafuni… ni wasiwasi!

b. Wakilisha kile kisichotarajiwa

Makala yako lazma iwe ya kipekee, inayofungua macho. Ushauri wako unatakiwa uwe wa kweli na wenye kusaidia.

Usiwanyime wasomaji wako yaliyomo. Wape ushauri kamili na wenye nguvu, ukarimu wako kwa wasomaji utawafanya wawe wasomaji na wateja waaminifu.

c. Tengeneza mfumo au fuata mfumo.

Kadri makala yako inavokua na mfumo mzuri ndivyo msomaji anavozidi kupata hamasa ya kuendelea kusoma. Angalia mwanzo, katikati, na mwisho wa kila sehemu unayoandika, na uunde mfumo unao ongozana.

d. Mwanzo na mwisho uwe mzuri

Kama vile utangulizi wako na hitimisho zinaweza kunyakua wasomaji, pia unatakiwa maelezo ya makala yako yaanze na kumalizia vivyo hivyo. Wafanye wasomaji wajiskie hamasa wanapomaliza kusoma makala yako.

 

4. Kufunga au kumaliza makala

Kama wasomaji wako umewapa kichwa cha habari, utangulizi na maelezo yalio mazuri, basi hun budi kuwapa mwisho ulio mzuri. Usitake wasomaji wako wajute kwanini walisoma makala yako. Wape kitu cha kuchukua.

Hamasisha wasomaji wako

Waonyeshe kuwa wamefika mbali, wana uwezo gani, na ni maisha gani yataonekana kama tu watatumia ushauri wako. Wafanye waone kwamba haijalishi wameona nini au wamehangaika sana, lakini wakati wao ni sasa.

 

Hitimisho kiujumla

Umekamilisha makala yako, chukua mda kupumzika, rudi kuipitia tena makala yako baada ya mapumziko kama msomaji.

Ukisha maliza kupitia makala yako fanya matengenezo, boresha makala yako, unaweza kuongeza picha, video, na viambatanisho vingine vinavyoweza kufanya makala yako ivutie kwa msomaji, ukiona ipo tiari unaweza kuchapisha makala yako.

Na hivi ni kwa ufupi jinsi makala ya Kitaalam inavoandikwa.

  1. Chagua mada na uandike kichwa cha habari
  2. Andika utangulizi mzuri
  3. Orodhesha vidokezo vichache
  4. Andika hitimisho la makala yako
  5. Hariri na rekebisha na tengeneza
  6. Chapisha

Ukitumia njia hii na kuongezea ubunifu wako, hautapata shida katika kuandika makala yako. Kama ni mara yako ya kwanza kuandika makala njia hii itakufanya uwe mtaalam kwenye tasnia hii ya kuandika makala.

Haitokuwa rahisi kila wakati, ila utakuwa na muundo wakati utakapokwama. Fanya mazoezi kila wakati mwishowe utaanza hisi ni kawaida.

Je wewe unaandikaje makala? Je unaweza tuambia maendeleo yako katika uandishi wa makala? Shiriki katika maoni.

Report

What do you think?

Written by Swahilify

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *


The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.

Vidokezo vya kufanya Kompyuta yako kuwa salama.