in ,

CoolCool CuteCute

Msitu wa Amazon

Msitu huu unatambulika pia kama Amazonia au Pori la amazon ambao upo katika eneo la Amerika ya Kusini. Msitu huu ni mkubwa sana wengi husema ni wa kwanza lakini ni msitu mkubwa kuliko yote duniani kwa misitu yenye mvua za kitropiki (tropical rainforest) na wa pili ukijumuisha misitu ya aina zote duniani ukiongozwa na msitu wa Taiga.

Upo nchi gani?

Msitu huu kisayansi unasemakana ulikuwepo tangu miaka millioni 59 iliopita. Ukiwa na kilometa za mraba 5,500,000. Na umeenea katika nchi tisa za Amerika ya kusini ambapo asilimia 58.4% kuwemo nchini Brazil, na nchi zingine nane ikiwemo Peru kwa 12.8%, Bolivia kwa 7.7%, Colombia 7.1%, Venezuela 6.1%, Guyana 3.1%, Suriname 2.5%, French Guyana 1.4% na Ecuador 1%.

Mito

Msitu wa amazon umejaa maelfu ya mito ukiwemo mto amazon, ambao unasifika kwa kuwa na maji mengi kuliko yote duniani yaani humwaga zaidi ya lita 200 kwa sekunde kwenye bahari ya Atlantic. Na ni mto wa pili kwa urefu duniani wenye kilomita 6840. Mto huo unaweza kutiririka kilomita 120 hadi kuchanganyika na maji ya chumvi wakati uingiapo baharini.

Viumbe Hai

Aslimia 10% ya viumbe hai duniani huishi katika msitu huo wa Amazon, ni nyumbani kwa aina za wanyama, mimea, wadudu, samaki, zaidi ya millioni 10. Kuna spishi karibu 40,000 za mimea, spishi za ndege 1,300, aina 3,000 za samaki, mamalia 430 na wadudu tofauti wa milioni 2.5. Cha kufurahisha zaidi kuna aina za matunda zaidia ya 3000.

Karibu kabila 400-500 za asili za Wamarekani huita msitu huu wa mvua wa Amazon nyumbani. Inaaminika kwamba karibu kabila hamsini za hawa hawajawahi kuwasiliana na ulimwengu wa nje.

Hatari kwenye msitu huo

Pamoja na vivutio vingi msitu huu pia ni nyumbani mwa wanyama wanaoweza kukusababishia kifo, kama mkunga mwenye umeme (electric eel), samaki wanaokula nyama (piranhas), vyura wenye sumu, chui na nyoka wakubwa na wenye sumu kali.

Hali ya Hewa.

Sehemu hii ya uzuri mkubwa wa asili ina jukumu muhimu katika kupunguza mabadiliko ya hali ya hewa. Hii ni kwa sababu mimea yenye utajiri huchukua kaboni dioksidi (Carbon dioxide CO2 – gesi chafu) kutoka kwenye hewa na huachia oksijeni (Oxygen O2 – gesi safi) kwenye hewa.

Kwa sababu ya unene wa dari (matawi ya juu na majani ya miti), sakafu ya Amazon iko gizani milele. Kwa kweli, ni nene kiasi kwamba wakati kunanyesha, inachukua karibu dakika kumi kwa maji kufikia ardhi.

Mfuko wa Wanyamapori Ulimwenguni (WWF) unaripoti kwamba kiwango cha haraka cha ukataji wa miti kinachotokea katika eneo la Amazon kinaweza kusababisha mabilioni ya tani za kaboni ambazo ambayo kwa sasa huifadhiwa au kuchukuliwa na mimea katika msitu huo kuachiwa

Unafahamu nini kuhusu msitu huu? Toa maoni yako kwenye koment hapo chini.

This post was created with our nice and easy submission form. Create your post!

Report

What do you think?

Written by Profeseli

2 Comments

Leave a Reply

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *


The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.

Ndege iliyopotea kutokea baada ya miaka 37

Fahamu kuhusu Kobe Bryant