Mto Mississippi – Missouri (4/6)

List item
Approved

Mto Missouri ni mto mrefu zaidi katika Marekani ya Kaskazini. Hutoka katika Milima ya Rocky ya magharibi mwa Montana, Missouri inapita mashariki na kusini na kuwa na urefu wa kilomita 3,767 (2,341 mi)  kabla ya kuingia Mto wa Mississippi kaskazini mwa St. Louis, Missouri.

Mto wa Mississippi ni mto wa pili  kiurefu na mto mkuu wa mfumo wa pili wa mifereji ya maji kwenye bara la Marekani ya Kaskazini. Kutoka chanzo chake cha asili cha Ziwa Itasca kaskazini mwa Minnesota, kwa kawaida inapita kusini na kuwa wenye urefu wa kilometa 3,730 (2,320 mi) hadi Delta ya Mto huo kwenye Ghuba ya Mexico.

Jumla ya urefu wa mito hii miwili ambayo huunganika na kuwa kitu kimoja ni kilometa 6,275 (3,902 mi). Ambapo huitwa Mto Mississippi.

Written by Profeseli

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.

Mto Yangtze (3/6)

Mto Yenisei (5/6)