Msitu huu unatambulika pia kama Amazonia au Pori la amazon ambao upo katika eneo la Amerika ya Kusini. Msitu huu ni mkubwa sana wengi husema ni wa kwanza lakini ni msitu mkubwa kuliko yote duniani kwa misitu yenye mvua za kitropiki (tropical rainforest) na wa pili ukijumuisha misitu ya aina zote duniani ukiongozwa na msitu wa Taiga.
Upo nchi gani?
Msitu huu kisayansi unasemakana ulikuwepo tangu miaka millioni 59 iliopita. Ukiwa na kilometa za mraba 5,500,000. Na umeenea katika nchi tisa za Amerika ya kusini ambapo asilimia 58.4% kuwemo nchini Brazil, na nchi zingine nane ikiwemo Peru kwa 12.8%, Bolivia kwa 7.7%, Colombia 7.1%, Venezuela 6.1%, Guyana 3.1%, Suriname 2.5%, French Guyana 1.4% na Ecuador 1%.
Mito
Viumbe Hai
Aslimia 10% ya viumbe hai duniani huishi katika msitu huo wa Amazon, ni nyumbani kwa aina za wanyama, mimea, wadudu, samaki, zaidi ya millioni 10. Kuna spishi karibu 40,000 za mimea, spishi za ndege 1,300, aina 3,000 za samaki, mamalia 430 na wadudu tofauti wa milioni 2.5. Cha kufurahisha zaidi kuna aina za matunda zaidia ya 3000.
Karibu kabila 400-500 za asili za Wamarekani huita msitu huu wa mvua wa Amazon nyumbani. Inaaminika kwamba karibu kabila hamsini za hawa hawajawahi kuwasiliana na ulimwengu wa nje.
Hatari kwenye msitu huo
Pamoja na vivutio vingi msitu huu pia ni nyumbani mwa wanyama wanaoweza kukusababishia kifo, kama mkunga mwenye umeme (electric eel), samaki wanaokula nyama (piranhas), vyura wenye sumu, chui na nyoka wakubwa na wenye sumu kali.
Hali ya Hewa.
Sehemu hii ya uzuri mkubwa wa asili ina jukumu muhimu katika kupunguza mabadiliko ya hali ya hewa. Hii ni kwa sababu mimea yenye utajiri huchukua kaboni dioksidi (Carbon dioxide CO2 – gesi chafu) kutoka kwenye hewa na huachia oksijeni (Oxygen O2 – gesi safi) kwenye hewa.
Kwa sababu ya unene wa dari (matawi ya juu na majani ya miti), sakafu ya Amazon iko gizani milele. Kwa kweli, ni nene kiasi kwamba wakati kunanyesha, inachukua karibu dakika kumi kwa maji kufikia ardhi.
Unafahamu nini kuhusu msitu huu? Toa maoni yako kwenye koment hapo chini.