in ,

CoolCool

Vidokezo vya kufanya Kompyuta yako kuwa salama.

Kadri miaka inavozidi kwenda, Kompyuta na Simujanja vimekuwa muhimu katika maisha yetu ya kila siku. Tunavitumia katika kazi zetu, majumbani na pia katika sekta za elimu.

Matumizi ya kompyuta yanavozidi kuwa makubwa, ndivyo zinavozidi kuwa hatari zaidi. Linapokuja suala la usalama wa kompyuta, vitu vingi hatarishi inabidi vitiliwe manani.

Vitu hivo ni kama Programu mbaya (Malicious Software), Virusi (Virus), Trojans na kadhalika ambavyo vinatumiwa na hackers ili kuharibu, au kupata taarifa za mtumiaji wa kompyuta.

Shida ni kwamba watu wengi hawana mda au hawana mpango kufanya kompyuta zao kuwa salama. Mara nyingine inaweza kuwa njia unazopewa ni ngumu kuelewa au ni gharama kubwa kutumia.

Bahati nzuri, kuna hatua unazoweza kuchukua ili kupunguza hatari ya kuathiriwa na kompyuta yako. Natumai kukupa mwanzo kurahisisha mambo. Ninasema “mwanzo” kwa sababu, usalama wa kompyuta ni mada kubwa na kampuni nyingi kubwa hutumia mamilioni ya dola kila mwaka.

Kwa mtumiaji wa kawaida, ukichukua hatua hizi kadhaa za kimsingi inapaswa kuwa njia ya kutosha kuiweka kompyuta yako na yaliyomo salama.

1. Weka kompyuta yako ikiwa imesasishwa (Updated)

Programu unazozitumia zinaweza kuonekana kama kero katika kuleta updates, ni jambo muhimu kuhakikisha uko sambamba na updates zote zilizotoka. Mbali na kuongeza huduma za ziada, mara nyingi hurekebisha maswala ya usalama.

Idadi kubwa ya hacks zinatokea baada pale ambapo mashimo ambayo watengeneza programu waliyafunga endapo miezi au hata miaka iliyopita.

Hata ingawa kawaida ni jambo zuri, ni busara kuwa mwangalifu kuhusu updates. Wakati mwingine kampuni za programu zitatoa matoleo ya kabla kwa ajili ya majaribu. Hizi zinaweza kuwa zisizo salama na zinapaswa kutumiwa kwa hiari yako mwenyewe.

Jambo lingine la kutazama ni updates bandia (fake). Hizi zinakuwa zinachapishwa na hackers ili kukufanya upakue programu hatarishi. Unaweza kuzuia hivi kwa kufanya unchunguzi kutoka kwenye kampuni ya hio programu.

2. Washa au weka Firewall

Sijapata jina au neno la Firewall kwa kiswahili kama unalifahamu unaweza ukanisaidia kwenye comments hapo chini.

Firewall ni nini? Hii ni programu ambayo inachambua au huwa kama kizuizi cha mawasiliano kati ya kompyuta yako na mtandao.

Kama kompyuta yako imekuja na firewall (Windows XP kuja juu, Mac nk.) basi cha kufanya ni kuangalia kama imewashwa. Ila kama haina au unahisi unahitaji programu ambayo itafanya hio kazi basi unaweza jaribu Zone Arlam, Comodo, na TinyWall ambazo zinapatikana bure.

3. Weka programu ya kupambana na Virusi (AntiVirus)

Wengi wetu tunachanganya kwa kufananisha Firewall na Antivirus, ila hizi ni program mbili tofauti na kila moja inafanya kazi za aina tofauti, ila zote zinatimiza lengo moja ambalo ni usalama.

AntiVirus ni nini? Hii ni programu ya kompyuta inayotumiwa kuzuia, kugundua, na kuondoa virusi vya kwenye kompyuta.

Je AntiVirus ni kupoteza muda tu, uangalifu wako unatosha na kwamba yote programu hio inachofanya ni kupunguza kasi kompyuta yako?

Ukweli ni kwamba, ndio AntiVirus inapunguza kasi ya kompyuta yako, lakini bora kasi ya kompyuta yako ipungue kuliko, kuingiliwa na Virusi kwenye kompyuta yako.

Je kampuni za Antivirus ndizo zinatengenza virusi ili kujiongezea kipato?

Kampuni za antivirus hawatengenezi virusi, wapo hackers wengi duniani ambao wanatengeneza virusi kwa ajili ya kukuibia na kupata taarifa zako.

Kati ya Antivirus nzuri za bure ni Windows Defender au Windows Essential ambayo inapatikana kwenye kompyuta za Windows. AntiVirus zingine maarufu ni Bitdefender, Avast, Kaspersky, na nyingine nyingi.

4. Rekebisha utumiaji wa Kivinjari (browser) chako.

Kivinjari (browser) unayotumia na jinsi unavyokitumia inaweza kuwa sababu ya Kompyuta yako kuwa na virusi.

Vivinjari vingi vina chaguzi ambazo hukuwezesha kurekebisha kiwango cha faragha na usalama wakati wa kuvinjari. Hivo zinaweza kusaidia kupunguza hatari ya maambukizo kufikia kompyuta yako na hackers wanaoshambulia kifaa chako.

Je ni nini naweza fanya kuepukana na virusi mtandaoni?

  • Jitahidi kufungua tovuti lengwa, ile ambayo unadhumuni ya kulifungua.
  • Penda kutembelea tovuti zenye https au kikufuli, huwa zinakuwa salama zaidi.
  • Epuka kupakua (downlaod) mafaili usiyotambua, na hakikisha kile unacho pakua kinakaguliwa na Antivirus, kabla ya kukifungua.
  • Pakua plugin (programu-jalizi) ambazo zitasaidia kuzui vifuatiliaji. Tembelea tovuti husika Chrome, Mozilla Firefox, nk.

Je ni Kivinjari (browser) gani ni bora Kutumia?

Kila mtu ana kile akipendacho ni kama hoja ya Android na iPhone haitokaa kuisha, mimi binafsi napendekeza Chrome, Mozilla, na Brave.

Kama unataka vivinjari (browser) ambavyo vipo salama zaidi, unaweza tumia Tor Browser, Epic, Comodo Dragon na Brave.

Pia unaweza tumia VPN wakati unaingia mtandaoni ili kuwa salama zaidi.

5. Tumia nenosiri imara.

Nenosiri ni safu ya maneno ambayo yanaweza kuwa herufi, namba na alama, ambayo inakupa ruksa ya kufikia kompyuta au huduma ya mtaondaoni nk.

Wakati hatua nyingi za usalama zinahusiana na vitisho visivyoonekana, wakati mwingine kuna uwezekano mtu akaweza kufikia kompyuta yako kwa mikono. Njia rahisi hapa ya kuiweka Kompyuta salama ni kuweka nenosiri kali kwenye kompyuta yako.

Je neno siri gumu linakuaje?

  • Tumia herufi kubwa na ndogo kwa wakati mmoja
  • Tumia herufi (A-Z), Namba (0-9) na alama (/@#\!). Yote kwa ujumla yasiwe chini ya 8.
  • Usitumie maneno ambayo ni rahisi kuotewa, tarehe yako ya kuzaliwa, jina lako peke yake.
  • Kama huwezi kushika nenosiri unaweza tumia Google Password Manager kuhifadhi nenosiri zako.
  • Usimpe mtu yeyote nenosiri lako.

Hitimisho

Usalama wa kifaa chako au kompyuta yako ni wako mwenyewe. Kama unavoweza kulinda nyumba yako, basi tambua ya kuwa kifaa chako kinaweza kuwa kimeshikilia au kubeba vitu muhimu zaidi hata kuliko vilivyopo nyumbani kwako.

Kumbuka ya kuwa njia hizi ni mwanzo tu wa usalama wa kawaida. Kuna vitu vingine vingi ambavyo vinaweza kusaidia kuweka kifaa chako salama, maana tasnia ya usalama wa kompyuta na mtandao ni mpana sana.

Nama unaona huwezi kufanya hivyo au unahisi kompyuta yako imeathiriwa basi hunabudi kupata ushauri kutoka kwa mtaalam wa Kompyuta aiweke salama.
Usijaribu kufanya marekebisho bila kuwa na ujuzi kwani waweza poteza mafaili na taarifa zako za muhimu.

Je unatumia njia gani kulinda kifaa chako?

Report

What do you think?

Written by Swahilify

2 Comments

Leave a Reply

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *


The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.

Jinsi ya Kuandika Makala Kitaalam.

Jinsi makala inavoweza kukupatia kipato.