in ,

WTFWTF LoveLove CoolCool

Jinsi ya kupata hela kupitia Youtube

Umashuhuri kupitia Youtube umezidi kuwa mkubwa sana duniani. Nazungumzia watu ambao wamepata hadhira kwa kuunda yaliyokusudiwa kufundisha, kuburudisha, kukagua, na kuwa bora kwenye wavuti.

Kutengeneza kipato inaweza isiwe sababu yako ya kwanza ya kutengeneza kituo (channel) cha youtube. Lakini kwa kutumia ujuzi uliokua nao unaweza ukajipatia kipato na kuendeleza ujuzi wako.

Ni njia gani unaweza tumia kutengenza au kupata kipato kupitia youtube?

Zipo njia nyingi unaweza kujitengenezea kipato kwa kutumia Youtube na ikakulipa vizuri kuliko kazi yako ya kila siku. Watu wengine hutumia Youtube kama sehemu kubwa ya kipato chao cha kila siku tazama hapa. Hata wewe pia unaweza ukawa mmoja ya watu wanaojipatia kipato kizuri kupitia Youtube.

Katika makala hii nitakueleza njia mbali mbali za kutengeneza kipato kupitia mtandao wa youtube.

Kabla sijaendelea kufafanau njia hizo. Natumai kuwa una akaunti ya gmail inayoweza kukufanya uingie kwenye youtube na kuweza kurusha video zako.

1. Kuwa Youtube Partner (Mshirika wa Youtube)

Hii ni njia ya kawaida ambayo watu wengi hutumia kujipatia kipato kutoka youtube. Ni njia inayotumika na kutegemewa na wengi bila kutegemea njia nyingine tofauti.

Kuwa kwenye Programu ya Ushirika wa Youtube (Youtube Partner Program) inahitiji ukidhi vigezo na masharti ya Youtube ambayo ni kuwa na Subscribers 1000 na angalau masaa 4000 ya kuangaliwa kwa miezi 12 iliyopita, pia video unazozirusha ziwe zinafwata vigezo na masharti ya Youtube.

Utatakiwa kuwa na akaunti ya Adsense ili kufanikisha Ushirika. Kujiunga na adsense tembelea/bonyeza link hiii na ufwate maelekezo.

Kutaka kufahamu kuwa akaunti/chaneli yako ipo tayari kwa Programu ya Youtube tembelea Youtube Studio kisha upande wa kushoto tafuta Monetization.

Youtube inakupa uwezo na fursa mbali mbali za kujikuza kifedha. Kati ya mambo ambayo youtube hutoa ni;

Uanachama wa chaneli (Channel Membership) – Wanachama wako kufanya malipo yanayojirudia kila mwezi kupata dondoo kutoka kwako. Hii inahitaji uwe na subscribers zaidi ya 30,000.

Uuzaji wa bidhaa Youtube (Merchandise Shelf) – Uwezo wa kuudha bidhaa zako moja kwa moja kwa kutumia mfumo wa youtube. Utahitaji uwe subscribers 10,000.

Super Chat & Super Stickers – Hii huwapa watumiaji uwezo wa kulipia maoni yaliobandikwa (pinned comments) kwenye video zilizo live. Unahitaji kuwa katika nchi zinakubali super chats.

Mapato ya Youtube Premium – Pale ambapo mtumiaji wa Youtube Premium atakapoangalia video zako, nawe utakuwa umepata kipato.

* Ili kupata mapato yako unatakiwa uwe na umri si chini ya miaka 18. Au uwe na mlezi wa kisheria aliye na umri wa zaidi ya miaka 18 ambaye anaweza kushughulikia malipo yako kupitia AdSense.

Image Source: Freepik

2. Ushirika na Mitandao Mingine (Affiliate Marketing)

Hii ni kati ya njia moja rahisi ambayo watu wengi pia hutumia kupata kipato. Njia hii unaweza kuifanya kwa kuwapa watu tovuti za ushirka kwenye video yako sehemu ya maelezo ya video yako.

Mfano wa njia za ushirika, Kuelezea Bidhaa/huduma, Mapendekezo ya Bidhaa/Huduma, Kuorodhesha bidhaa/huduma/vifaa ulivotumia na wapi pakuvipata.

3. Uuzaji wa bidhaa/huduma yako mwenyewe.

Kama unayo bidhaa/huduma, unaweza tengeneza video zinazo onesha/kueleza bidhaa yako na kuziwasilisha Youtube. Utahitaji kuwa na tovuti au eneo la kuwaelekeza watazamaji wako kupata huduma kutoka kwako.

Pia kama huna bidhaa/huduma, unaweza tengeneza au kuunda bidhaa yako mwenyewe zitakazo wavutia watazamaji wako na kuwafanya kuwa na uhitaji. Mfano wa bidhaa hizo ni T-shirt, na bidhaa/huduma nyingine mbali mbali.

4. Tengeneza video zenye udhamini.

Kumbuka Youtube ni tovuti ya kijamii kama tovuti zingine. Hivyo kama unaweza kudhamini bidhaa/huduma fulani kwenye mtandao wako wa Instagram, facebook nk. basi vivyo hivyo waweza fanya kupitia Youtube.

Tafuta kampuni au biashara zinazoweza kubali kukudhamini na urushe video zako zikiwa zimedhaminiwa. Kumbuka kama utakuwa na wafuasi pamoja na watazamaji wengi kwenye chaneli yako basi itakuwa rahisi kwako kupata wadhamini.

5. Ufadhili wa Chaneli yako.

Njia nyingine unaweza kupata kipato kupitia youtube ni kwa kutumia njia za ufadhili. Njia hii imejulikana kuwa njia rahisi kwa kuwafanya watazamaji kuingia kwenye mifuko yao wenyewe na kukufadhili.

Tafuta tovuti/sehemu ambayo itakuwa rahisi kwa watu kutoka sehemu mbali mbali kuweza kutuma michango yao bila ya kuwa na mlolongo mrefu. Pia ni rahisi sana kupata ufadhili kama huduma unayotoa inalenga jamii na kuigusa kwa mapana yake.


Mtandao wa Youtube ni mpana sana wenye watumiaji wengi. Kama ilivyo kwa mitandao mingine ya kijamii. Kile unachokiwasilisha ndo kinaweza kuwa chachu ya mafanikio yako hadi kupata subscribers na watazamaji wengi.

Je una maoni gani kuhusu njia za kujipatia kipato kwa kutumia Youtube? Unatumia njia gani na njia ipi ni rahisi zaidi?

Report

What do you think?

Written by Swahilify

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *


The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.

Jinsi ya kutengeneza tovuti bila ujuzi wowote

Milima Mirefu Duniani (Top 5 Kila bara)