in ,

CoolCool

Jinsi ya kutengeneza tovuti bila ujuzi wowote

Wengi tumekuwa tukitamani kuwa na tovuti kwa sababu mbali mbali iwe biashara au binafsi. Ila swala linalowakumba wengi ni jinsi ya kuwa na tovuti hio.

Wengi tumekuwa tukiwaza jinsi ya kutengeneza tovuti kwa ajili ya biashara na kushindwa. Labda kwa namna moja au nyingine gharama ya kumpata mtaalam akutengenezee tovuti ni kubwa sana au mtaalam unaemtafuta yuko mbali na eneo lako la kazi.

Je unafahamu ya kuwa unaweza tengeneza tovuti bila kuwa na ujuzi wowote?

Kama unaweza kutumia kompyuta kuandika vitu mbalimbali kama viwasilishi (presentation) nk. Basi pia unaweza tengeneza tovuti yako kwa elimu ya utumiaji wa kompyuta tu.

Tovuti za utengenezaji au Kuajiri Mtaalam

Kwa kawaida kuajiri mtaalam inaweza kuwa gharama kidogo, makadirio ya kuanzia $400 na kuendela. Kadri mahitaji ya tovuti yako yanavozidi kuwa makubwa ndivyo gharama huongezeka. Hivyo usishangae ukiambiwa kiasi cha $1000 au zaidi.

Lakini kwa kutumia tovuti za utengenezaji (website builders) unaweza ukatengeneza tovuti yako kuanzia kiasi cha chini cha makadirio yaani robo ya ile ambayo ungemtumia mtaalam.

Tovuti za utengenezaji ni nzuri kwa ajili ya.-

Biashara Ndogo, Watu binafsi, Waandishi, Wasanii, Wapiga Picha nk.

Katika Makala hii nitakuonesha sehemu (tovuti) kadhaa unazoweza kwenda na kutengeneza tovuti yako bila ya kuwa na utaalam wowote.

Wix

Hii ni tovuti maarufu ambayo ina kupa urahisi na uhuru wa kutengeneza tovuti yako mwenyewe. Inakupa orodha nyingi za muonekano ambazo utaweza chagua ile ambayo inafaa biashara yako.

Kwa kuongeza, Wix hutoa chaguzi tatu tofauti ambazo unaweza kuchagua; ADI, Editor na Code. ADI ni mfumo utakao kuuliza maswali ili kutengenezea muundo utakaokufaa, wakati Editor hukupa uhuru zaidi ambapo utachagua muundo wako mwenyewe. Wakati huo huo, Code ni kwa watumiaji wenye utaalam ambao wangependa kuunda nafasi zaidi. Chaguzi mbili za mwanzo hazihitaji ujuzi wowote!

Bonyeza link hii kuone tovuti zilizotengenezwa na wix.

Weebly

Weebly ni mjenzi wa tovuti rahisi ambayo inahitaji kazi kidogo kwako kukamilisha ukurasa wako mzuri. Weebly inaweza tengeneza miundo ya tovuti za aina mbali mbali ila imejikita zaidi kwenye mfumo wa uuzaji mtandaoni.

Weebly inatoa pia nafasi ya kurusha tovuti yaani (subdomain) chini ya tovuti yao bure kwa kuzingatia vigezo na masharti yao. Mfano: swahilify.weebly.com.

Site123

Site123 ni kati ya tovuti zinazokupa urahisi wa hali ya juu. Wakati zingine zinakupa chaguzi za kutengeneza muundo. Hii imekupa urahisi wa kupakia yaliyomo tu. Yaani wewe ni kuandika/kupakia picha nk. na tovuti yako inakua hewani.

Pia hii inakupa nafasi ya kurusha tovuti kwenye subdomain yao bure kwa kuzingatia vigezo na masharti ya Site123. Mfano: swahilify.site123.com.

Squarespace

Squarespace ni mjenzi wa tovuti ambaye ana mengi ya kutoa kwenye ubunifu na biashara. Sio rahisi kuitumia Squarespace, utahitaji muda zaidi na uvumilivu kuweza kuizoea na kuitumia kiurahisi.

Squarespace inavutia kabisa na miundo yake (template). Kama unahitaji tovuti yenye muundo mzuri na wa kuvutia basi squarespace inaweza kuwa chaguo bora kwenye biashara yako.

WordPress.com

WordPress.com ni kati ya tovuti kubwa za utengenezaji duniani. Watu wengi hutumia WordPress na tovuti nyingi mtandaoni hutumia WordPress. Pia kama unataka kuanzisha blog basi ushauri wangu ni uanze kutumia wordpress.com.

Si rahisi kutumia wordpress.com kama ilivyo kwa tovuti zingine. Ila ukiwa na utiari wa kujifuza zaidi unaweza kuitumia kiurahisi zaidi. Unaweza kujifunza zaidi kuhusu wordpress.com hapa.

Hitimisho

Kwa kutumia tovuti hizo unaweza kutengeneza tovuti yako bila kuwa na ujuzi wowote. Natumai kuwa unaweza ukawa unafahamu njia zingine rahisi zaidi, au njia/tovuti iliyo bora zaidi.

Tupia comment hapo chini kutujuza uyajuayo.

Report

What do you think?

Written by Swahilify

3 Comments

Leave a Reply

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *


The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.

Umuhimu wa Tovuti kwenye biashara.

Jinsi ya kupata hela kupitia Youtube