in ,

Jinsi makala inavoweza kukupatia kipato.

Katika makala iliyopita nilizungumzia jinsi ya kuandika makala kitalaam na tukaona makala nzuri ya kitaalam inavotakiwa kuandikwa.

Kama unavoweza kumfanya msomaji kufurahia makala yako vivyo hivyo katika makala hii tutaona jinsi unavoweza kutengeneza au kupata kipato kwa kuchapisha makala.

Pamoja na misingi hii unaweza kuwa tayari kuanza kujaribu kupata pesa/ kipato kutoka kwa blogi au uchapishaji wa makala yako lakini unahitaji kujua kuwa kwa sababu umeanzisha, umeridhika na umeshirikisha wasomaji. Hivyo basi pesa hazitojichuma zenyewe.

1. Matangazo (Advertisement)

Hapa ndipo waandika makala wengi hujipatia kipato. Wakati wasomaji na makala yako inavozidi kukua ndivyo utakavyopata kampuni au watu wanaotaka kutangaza kwenye blogi au makala yako kirahisi.

Unaweza kurusha matangazo binafsi, au unaweza kufanya kazi na mitandao ya matangazo (kama vile Google Adsense).

Tofauti kubwa kutoka kwa chaguo zilizotajwa hapo juu ni kwamba kwa matangazo binafsi hakuna mtu wa kati, ambayo inamaanisha unaweza kuweka viwango vyako vya tangazo. Na kwa kutumia mitandao ya Matangazo viwango huwekwa na Mitandao hio.

2. Mitandao ya Ushirika (Affiliate Marketing/Network)

Kuiweka kwa urahisi, affiliate network ni wakati unaunganisha bidhaa ambayo inauzwa kwenye tovuti nyingine na ikiwa mtu atafuata kiunga chako na kuishia kununua bidhaa au huduma hiyo unapata kiasi kwenye mauzo hayo.

Unaweza kutumia uuzaji wa ushirika kupitia mitandao ya Washirika, au unaweza kuunda ushirika wa kibinafsi na watangazaji na biashara na programu ya ushirika.

3. Uuzaji wa Bidhaa Mtandaoni (Selling Products)

Uuzaji wa bidhaa kwenye Makala yako ni njia nyingine ya kujipatia kipato, kwani waweza kuelezea bidhaa fulani ambayo unahisi itakua inahitajika na wasomaji wako na ukapata kuwauzia kwa njia ya mtandao.

Unaweza kuuza vitu kama Ebooks(Vitabu vya Mtandao), Picha, Video, Miziki, Nguo, nk. Tambua ya kuwa utaweza kuuza kitu kirahisi kulingana na jinsi wasomaji wako wanapoelekea.

Hitimisho

Kuna njia nyingi zinazoweza kukupatia kipato kwa uandishi wa makala kama vile Uuzaji wa Huduma, Makusanyo ya Michango, Kuuza Ushauri nk.

Hizo hapo juu nilizo orodhesha njia kuu chache ambazo waandishi wengi hutumia kujipatia kipato katika uandishi wa makala. Kadri wasomaji wanavozidi kwenye makala yako ndivo unavoweza kujipatia kipato kikubwa zaidi.

Natumai sasa umeweza tambua jinsi Makala inaweza kukupatia kipato.

Je unatumia njia gani kujipatia kipato kwenye Makala yako?

Unaweza kutuelezea mbinu unazotumia kujipatia kipato kwenye makala zako.

Report

What do you think?

Written by Swahilify

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *


The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.

Vidokezo vya kufanya Kompyuta yako kuwa salama.

Kheri ya Mwaka Mpya 2020