in ,

OMGOMG CoolCool CuteCute LoveLove

Milima Mirefu Duniani (Top 5 Kila bara)

Je unafahamu kuna milima mingapi duniani?

Takwimu zinaonesha kuwa kuna milima takribani 1,187,049 hapa duniani. Takwimu hizi zimetolewa na peakvisor.com

Kwakweli kuna milima mingi sana duniani. Maajabu mengi yameizunguka dunia hii na mengi bado hatuna taarifa nayo.

Hata hivyo unaweza ukawa unajiuliza kuwa mlima mrefu kuliko wote duniani ni upi. Ni swali rahisi kwa wengine lakini sote ni wanafunzi katika elimu ya dunia hii. Hivyo basi tambua ya kuwa mlima mrefu kuliko wote ni Mlima Everest wenye urefu wa Mita 8,848 sawa sawa na Futi 29,029, mlima huo umo barani Asia.

Sasa basi chapisho hili litakupa orodha ya milima mitano (5) mirefu katika kila bara duniani.

AFRICA

Mlima Kilimanjaro
  1. Mlima Kilimanjaro – Tanzania, Urefu = 5,895 m (19,341 ft)
  2. Mlima Kenya – Kenya, Urefu = 5,199 m (17, 057 ft)
  3. Mlima Stanley au Mlima Ngaliema – DR Congo/Uganda, Urefu = 5,109 m (16,762 ft)
  4. Mlima Speke – Uganda, Urefu = 4,890 m (16,040 ft)
  5. Mlima Baker – Uganda, Urefu = 4,844 m (15,892 ft)

ASIA

Mlima Everest
  1. Mlima Everest – Nepal/China, Urefu = 8,848 m (29,029 ft) [Namba 1 Duniani]
  2. Mlima K2 – Pakistan, Urefu = 8,611 m (28,251 ft)
  3. Mlima Kangchenjunga – Nepal/India, Urefu = 8,586 m (28,169 ft)
  4. Mlima Lhotse – Nepal/China, Urefu = 8,516 m (27,950 ft)
  5. Mlima Makalu – Nepal/China, Urefu = 8,485 m (27,838 ft)

AMERIKA YA KUSINI

Mlima Aconcagua
  1. Mlima Aconcagua – Argentina, Urefu = 6,961 m (22,841 ft)
  2. Mlima Ojos Del Salado – Argentina/Chile, Urefu = 6,893 m (22,615 ft)
  3. Mlima Monte Pissis – Argentina, Urefu = 6,793 m (22,287 ft)
  4. Mlima Hauscaran – Peru, Urefu = 6,768 m (22,205 ft)
  5. Mlima Cerro Bonete – Argentina, Urefu = 6,759 (22,175 ft)

AMERIKA YA KASKAZINI

Mlima Denali
  1. Mlima Denali – Alaska, Urefu = 6,190 m (20,310 ft)
  2. Mlima Logan – Canada, Urefu = 5,959 m (19,559 ft)
  3. Mlima Pico De Orizaba – Mexico, Urefu = 5,636 m (18,491 ft)
  4. Mlima Saint Elias – Alaska/Canada, Urefu = 5,489 m (18,009 ft)
  5. Mlima Popocatepetl – Mexico, Urefu = 5,410 m (17,749 ft)

ULAYA

Mlima Elbrus
  1. Mlima Elbrus – Urusi (Russia), Urefu = 5,642 m (18,510 ft)
  2. Mlima Shkhara – Georgia, Urefu = 5,201 m (17,064 ft)
  3. Mlima Ararat – Uturuki (Turkey), Urefu = 5,137 m (16,854 ft)
  4. Mlima Blanc/Bianco (Mont Blanc) – France/ Italy, Urefu = 4,809 m (15,778 ft)
  5. Mlima Rosa (Monte Rosa) – Switzerland, Urefu = 4,634 m (15,203 ft)

ANTAKTIKA

Mlima VInson
  1. Mlima Vinson Massif, Urefu = 4,892 m (16,050 ft)
  2. Mlima Kirkpatrik, Urefu = 4,528 m (14,856 ft)
  3. Mlima Elizabeth, Urefu = 4,480 m (14,700 ft)
  4. Mlima Markham, Urefu = 4,350 m (14,270 ft)
  5. Mlima Sidley, Urefu = 4,825 m (14,058 ft)

AUSTRALIA

Mlima Kosciuszko
  1. Mlima Kosciuszko, Urefu = 2,228 m (7,310 ft)
  2. Mlima Townsend, Urefu = 2,209 m (7,247 ft)
  3. Mlima Twynam, Urefu = 2,195 m (7,201 ft)
  4. Mlima Rams Head, Urefu = 2,190 m (7,185 ft)
  5. Mlima Etheridge Ridge, Urefu = 2,180 m (7,152 ft)

Report

What do you think?

Written by Profeseli

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *


The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.

Jinsi ya kupata hela kupitia Youtube

JINSI NA NJIA ZA KUANZISHA BIASHARA