in ,

CoolCool CuteCute LoveLove LOLLOL OMGOMG AngryAngry WTFWTF CryCry

Jinsi ya kutoa hotuba nzuri

Habari karibu tena katika tovuti ya Swahilify.

Kwenye makala hii tutazungumzia kuhusu hotuba, maana yake jinsi unavoweza kuiwasilisha kwenye hadhira husika. Je ni vitu gani vya kuzingatia ukiwa unataka kutoa hotuba nzuri? Karibu nikupatie muongozo kamili wa jinsi ya kutoa hotuba nzuri.

Hotuba ni nini?

Hotuba ni kile ambacho mzungumzaji anakiwakilisha mbele ya hadhira. Inaweza jenga mvutano au punguza mvutano. Mara nyingi mfumo huu hutumika kwenye mikutano ya hadhara, mikutano ya kampuni, uzinduzi nk.

Hivyo basi Hotuba ni Mazungumzo rasmi ambayo msemaji anawasilisha kwa maneno ya lugha yaliotamkwa mbele ya hadhira iliyokusanyika kwa kusudi lengwa.

Kabla hujatoa hotuba, jitahidi kutambua kile unachotaka kukiwakilisha hivyo fanya maandalizi. Jaribu kutumia njia zifwatazo za kuandaa hotuba

Maandalizi ya hotuba

1. Mada kuu : Hatua ya kwanza ya kuandaa hotuba ni kutambua au kuchagua mada ya kuzungumzia. Hii itakupa muongozo wa kufanya uchunguzi wa kile utakachokiongea. Kama umepewa mada na wahusika basi unaweza kwenda kwenye kipengele kinachofwata.

2. Maandalizi : Baada ya kuitambua mada, sasa unaweza kukusanya taarifa kutoka sehemu mbalimbali kuhusu mada hio, na uhakikishe taarifa unazokusanya ni sahihi. Weka mpangilio wa kile ulichokiandaa kwa mtiririko unaohusiana.

3. Njia ya uwasilishaji : Wengi baada ya maandalizi tunasahau jinsi ya kuiwasilisha hotuba.. Kukumbuka hatua hii inaweza kuipa hotuba yako ladha nzuri kwa wasikilizaji/watazamaji. Unaweza kuiwaslisha kwa kusoma kile ulichokiandika kwenye maandali au ukakikariri au kutoa hotuba bila maandalizi. Pia unaweza ukatumia vifaa vya kiteknolojia kama vile Projector, Picha nk

4. Uchambuzi wa watazamaji/wasikilizaji : Kutambua hotuba ulioandaa kuwa umeiandaa kwa ajili watu gani, hali, mhemko, sehemu, nk. kabla na wakati wa kuiwasalisha itakupa uhuru na muongozo wa jinsi unavoweza kuiwasilisha hotuba hio.

Baada ya kupata muongozo na kujua nini maana ya hotuba na jinsi unavoweza kujiandaa kwa ajili ya hotuba sasa sina budi ya kuwaeleza mambo ya kuzingatia katika kuiwakilisha hotuba hio.

Uwasilishaji wa hotuba.

1. Nenda zaidi ya kushika umakini wa watu : Wakati kusudi lako la kutoa hotuba linaweza kuwa dhahiri kwako, watazamaji/wasikilizaji huwa wanafwata muelekeo wako. Hivyo miliki uwanja huo maana wewe ndo mtaalam. Unaweza jiuliza maswali haya,
Ni hisia gani nawapa wasikilizaji/watazamaji wangu? Msukumo, motisha, kuwezeshwa, kuelewa au kufahamu?
Je! Ni nini nataka wasikilizaji/watazamaji wangu wajue?
Je! Ninataka wasikilizaji/watazamaji wangu wafanye nini?

2. Tumia hisia na mantiki kuhamasisha : Lengo lako la kwanza ni kupata mtu/watu, mahali pengine kutenda tofauti. Kamwe usipoteze lengo hili. Watu wengi hufikiri vibaya kwa kuwaaminisha watu kwa kutumia data za machati, graphu na majedwali. Lakini ikiwa utatangaza hisia za kweli, unayo nafasi ya kushinda imani na uaminifu wa watazamaji wako.

3. Zingatia maneno yako ya kwanza : Sio jambo geni ila maoni ya kwanza yanazingatiwa sana. Kama unaanza kutetemeka wakati unaanza unaweza ukavuta pumzi nzito na kuanza. Unahitaji kunyakua watazamaji wako mara moja kwa kuwajulisha wewe ni nani na unajua nini.

4. Zingatia mkao wako : Mkao wako ukiwa dhaivu, ujumbe wako pia utatathminiwa na kuonekana kwa watazamaji wako kwamba umekosa kujiamini. Simama wima na kama, kuna uwanja mkubwa basi waweza kuzunguka kwa ustaarabu.

5. Toa Hadithi : Hadithi zinaunda kumbukumbu na nguvu ya kukaa kwa sababu zinaunganisha hisia na matukio. Hadithi yako inaweza kuungana na watazamaji wako milele kwa kuwaruhusu kuhisi kile unachohisi, kuona kile unachokiona na kuelewa kile unachoelewa kupitia maoni yako.Watazamaji wako wanaweza wasikumbuke mengi uliozungumza; Walakini, watakumbuka hadithi iliyotengenezwa vizuri.

6. Fanikisha kwa kuwa wewe : Wakati yote mengine yanashindwa, kuwa wewe. Fika mapema, wasalimie wale waliopo sehemu hio badilishana nao mawazo. Badala ya kuiga ya wengine, zingatia uwezo wako mwenyewe. Fanya ujuzi na vipaji vyako viangaze. Unapokua na shaka punguza kasi na uache akili yako ifanye kazi. Unaweza sema maneno kama “…fikiria hilo kidogo…” ili kuwa kituo kwa wasikilizaji huku wewe mwenyewe unapangilia maneno yako.

Katika hayo jitahidi kuweka mazungumzo yako kuwa mafupi. Na umalize kwa nguvu, haya ndio watazamaji makini hutilia manani.

Kutoa hotuba ni fursa ya kipekee katika maisha. Mda mwingine inaweza kukupa uwoga au msukumo wa kutojiamini. Ukijiandaa vizuri unaweza kutoa hotuba ya nzuri sana. Chukua vidokezo hivi na mara nyingine ukisimama kutoa hotuba natumai itakua ya kipekee.

Report

What do you think?

Written by Swahilify

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *


The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.

Faida za mitandao ya kijamii kwenye biashara.

Ndege iliyopotea kutokea baada ya miaka 37