in , ,

OMGOMG CryCry CoolCool

Ndege iliyopotea kutokea baada ya miaka 37

Wengi tumeskia kuhusu habari za ndege zilizopotea lakini hatujui mpaka sasa ndege hizo zimeenda wap. Je unafahamu kuhusu ndege iliyopotea na kuja kutokea miaka 37 baadae.

Wengi tumesikia kuhusu habari za ndege hio, na mitandao mbali mbali imekua ikisambaza taarifa kuhusu ndege hio. Mimi na wewe hatujui nini kilitokea na hatujui kama habari hio ni ya kweli au la. Basi tutachambua taratibu kuhusu hii habari tuutathmini ukweli kuhusu tarifa hii.

Taarifa kuhusu ndege hio inasemakana zimetolewa na shahidi ambae alikua ni muongoza ndege kwenye kiwanja cha ndege huko Caracas Venezuela aitwae Juan de la Corte.

KilichotokeaChapisho kuhusu ndege hio

Shahidi huyo anasema ni jambo la kushangaza sana kwa taswira alioshuhudia. Anasema ndege hio iliotua ilikua imechoka na ya kizamani sana kiasi kwamba ilishindwa kuonekana katika mitambo yao ya rada. Aliamua kuchukua hatua ya kuwasiliana na rubani kupata maelezo ya kuhusu ndege hio. Rubani akajibu ndege hio ni ya kukodi (charter plane) flight 914 yenye wafanyakazi wanne (4) na abiria hamsini na saba (57), na ilitakiwa kuwasili Miami kutokea New York. Taarifa hiyo ikawafanya wafanyakazi kwenye mnara wa uongozi (control tower) kupigwa na butwaa.

Juan akamuuliza yule rubani, Umepotea? Maana kule alipokua akieleka na hapo alipo ni kilomita 1800, na kumwambia kuwa pale alipo ni Caracas Venezuela, Amerika ya Kusini. Ndipo cha kustaajabu zaidi kikatokea wafanyakazi wa kwenye mnara wa uongozi wakasikia marubani wa ndege hio wakiwa wakishangaa mazingira ya sehemu hio. Rubani yule akauliza Tupo wapi? Nini hiki kimetokea? wakasema “Ndege hii inatakiwa kutua Miami saa tatu na dakika 55 ya tarehe 2 Julai 1955”  wakaambiwa hapa ni Caracas Venezuela tarehe 21 May 1992.

Wakati marubani wakiwa wanashindwa kuelewa nini kinaendela Juan akawatuliza na kuwaambia kuwa wafanyakazi wa ardhi (ground staff) wanakuja kuwapa taratibu, huduma na muongozo mwingine. Kufanya uchunguzi wakagunudua kuwa ni ndege ile ile ya mwaka 1955 cha kushangaza zaidi hawajakua hata kidogo.

Wakati wafanyakazi wa chini walipokaribia ndege hio, rubani akawaambia wafanyakazi hao warudi nyuma na wasiwasogelee na kuwaambia Tunaondoka Tena. Wafanyakazi hao wakaona sura za abiria zenye mshangao wakichungulia dirishani na rubani kutupa kalenda ya mwaka 1995. Na kuondoa ndege, hawakuonekana tena baada ya hapo.Kalenda aliyoacha rubani wa  ndege hio

Hiyo ndo taarifa inayotambulika kuhusu ndege hio. Taarifa zingine husema kwamba mjadala uliorekodiwa baina ya rubani na uongozi wa kiwanja hicho umepelekwa katika vyombo husika na unafanyiwa uchunguzi.

Uchunguzi Nliofanya.

Kiukweli nimefanya uchunguzi kiasi maana hamna taarifa za kiofisi zinazohusiana na hio ndege iliyopotea. Unaweza sema labda au namna moja au nyingine taarifa za ndege hio hufichwa na vyombo mbalimbali.

Nimekuja kugundua kuwa ndege hio pia haipo kwenye orodha ya ndege zilizopotea. Unaweza kupitia kwenye link hio chini.

https://en.wikipedia.org/wiki/List_of_missing_aircraft#1940%E2%80%931959

Kuna mambo mengi kuhusu hii ndege yanaonekana sio sawa, labda inaweza ikawa sababu ilikua miaka ya nyuma na kulikua hamna taarifa nzuri kuhusu swala hili. Kuna maswali unaweza kujiuliza na ushindwe kupata majibu. Mfano wa maswali unayoweza jiuliza. Familia za hao waiopotea ziko wap? Kwanini Caracas hawakutuma msako wa ndege hio? Mashahidi wengine wapo wapi?

Je unamawazo gani kuhusu hili? Toa maoni kupitia comment hapo chini.

This post was created with our nice and easy submission form. Create your post!

Report

What do you think?

Written by Profeseli

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *


The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.

Jinsi ya kutoa hotuba nzuri

Msitu wa Amazon