in , ,

Umuhimu wa Tovuti kwenye biashara.

Habari karibu tena kwenye tovuti yetu ya Swahilify.

Je unahitaji kuwa na tovuti kwa ajili ya biashara?

Hilo ni swali kila mtu mwenye biashara hujiuliza. Wengi tumekuwa hatujui umuhimu wa tovuti. Labda kwasababu majibu tuliokua nayo ni “gharama sana”, “inahitaji mda”, “teknolojia ngumu”, “nina biashara kubwa ya kutosha sihitaji moja”. Yote hayo yanaweza kukufanya usione umihumu wa kuwa na tovuti.

Ukweli ni kwamba huitaji kuwa na ujuzi sana wa teknolojia kuwa na tovuti. Unaweza kuwa na tovuti kiurahisi sana bila kuwa na ujuzi mkubwa na kwa bei rahisi vile hata usivotegemea.

Sasa je bado unajiuliza haja ya biashara yako kuwa na tovuti?

Kabla sijakupa mchanganuo wa umuhimu wa tovuti kwa ajili ya biashara yako nahitaji utambue kuwa asilimia zaidi ya 80% ya watu wenye uwezo ya kuingia kwenye mtandoa hufanya utafiti wa biashara mtandaoni

1. Hujenga Uaminifu

Je unafahamu ni vitu gani huleta uaminifu kwenye biashara. Ukiachana na mahali au eneo la biashara. Tovuti yako itajenga uaminifu kwa kusema, mimi niko hapa, ninamaanisha biashara, na niko kwa muda mrefu.
Kwa kupanga kwa uangalifu, kwa busara na kwa kuangalia mahitaji ya wateja wako, wavuti yako itatoa picha ya kitaalam na kuwapa wateja uwezo mkubwa wanapotembelea, iwe iko kwenye kompyuta zao, tableti au simu.

2. Huhifadhi Muda.

Muda ni pesa, kwa hiyo mara nyingi huunganishwa pamoja. Kuwasiliana na kutimiza haja wateja huchukua muda. Wavuti yako inaweza kuokoa muda huo kwa kutoa majibu ya maswali na maoni ya kawaida kwa wateja bila ya kurudia ujumbe huo huo kwa watu tofauti.
Unaweza kutumia wakati wako kufanya vitu vya thamani zaidi, kama kuendeleza biashara yako.

3. Hurahisisha upatikanaji wa Biashara yako.

Kuwa na tovuti hufanya iwe rahisi sana kwa watu kukupata, kusoma juu ya biashara yako, unachofanya na kujibu rundo la maswali waliyo nayo kwa ajili ya biashara yako. Kwa kuwa na tovuti watu wataweza kupata biashara yako wanapoitafuta kwenye injini za utaftaji kama google, yahoo au bing. Wakati mwingine mtu asipofanikisha kupata biashara yako mtandaoni anaweza akahis biashara yako imefungwa.

4. Fursa za kimataifa

Ukiwa na tovuti hufanya uwezekano kwa mtu yeyote ulimwenguni kupata biashara yako. Ikiwa unayo bidhaa/huduma ambayo inaweza kuuzwa kwa urahisi mtandaoni unaweza kuongeza kiwango kikubwa cha wateja wako kwa kuuza kwenye mtandao.

Au labda huwezi kuuza huduma/bidhaa zako mkondoni lakini kwa kuwa na wavuti unaweza kupata wateja ambao wako nje ya mahala pako kijiografia.

5. NI BEI RAHISI

Wengi hudhani kama kuwa na tovuti ni gharama sana. La hasha unaweza kuwa nayo kwa kiasi kidogo tu, tunaweza sema labda kwasababu ya kuhitaji tovuti yenye yaliomo yanayohitaji utaalam mkubwa, la sivyo usiweke picha akilini kwako kwamba kuwa na tovuti ni gharama.

Pia kuwa na tovuti sio tu kwa ajili kuonyesha kile unachotoa, ni sehemu ya Mkakati wa Uuzaji. Ukilinganisha na aina mbali mbali za mikakati ya uuzaji basi utagundua kuwa Uundaji au kuwa na tovuti ni bei nafuu zaidi.

Kujua zaidi juu ya kuwa na tovuti bonyeza hapa kuuliza jinsi ya kuwa na tovuti. Tutakuongoza kabisa hatua kwa hatua juu ya jinsi ya kuwa na tovuti yako.

Je! Nakala hii imekusaidia? au tumesahau kitu? Unaweza piga kura na kushiriki kwa maoni hapa chini.

Report

What do you think?

Written by Swahilify

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *


The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.

Mito Mirefu Duniani (Top 5)

Jinsi ya kutengeneza tovuti bila ujuzi wowote